Uhuru, viongozi wengine wakutana nchini Angola

Martin Mwanje
1 Min Read

Rais Mstaafu Uhuru Kenyatta leo Jumanne amejumuika na viongozi wa nchi na serikali wa kikanda na wataalam kuhudhuria mkutano wa pande nne unaotafuta namna ya kutatua mzozo uliopo mashariki mwa Jamhuri ya Demokrasia ya Congo, DRC.

Uhuru ndiye anayeongoza Mchakato wa Nairobi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, EAC juu ya Urejeshwaji wa Amani na Uthabiti mashariki mwa DRC. 

Pande husika kwenye mkutano unaoandaliwa mjini Angola ni EAC, Jumuiya ya Kiuchumi ya Mataifa ya Katikati mwa Afrika, Mkutano wa Kimataifa wa Eneo la Maziwa Makuu na Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika, SADC, pande zote zikikutana chini ya mwavuli wa Umoja wa Afrika.

Mkutano huo utaangazia namna ya kumaliza mzozo unaoshuhudiwa mashariki mwa DRC.
Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *