Serikali ya Uholanzi itashirikiana na kaunti zote 47 nchini kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia nchi.
Eneo la kiuchumi la kanda ya Ziwa ni sehemu ya maeneo ambayo yanafadhiliwa na serikali ya nchi hiyo.
Hii ni kwa mujibu wa Gavana wa kaunti ya Vihiga Dr. Wilber Otichillo aliyeyasema haya alipokuwa mwenyeji wa Balozi wa Uholanzi nchini Marten Brouwer katika makao makuu ya kaunti hiyo.
Dr. Otichillo alisema Uholanzi imehusika katika mipango kadhaa ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi nchini.
Wakati wa mkutano kati yao, wawili hao walijadili masuala kadhaa ikiwa ni pamoja na maji na usafi na namna ya kuboresha usambazaji maji.
Kadhalika walikubaliana jinsi ya Uholanzi inaweza ikaunga mkono usalama wa chakula kwa kuunga mkono kilimo kupitia kilimobiashara na kuwahusisha vijana kama njia ya kubuni ajira.
Uholanzi ni moja ya nchi ambayo imeshirikiana na Denmark na Benki ya Dunia kufadhili kaunti 47 kuhusiana na namna ya hasa kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.