Euro 2024: Uhispania na Uingereza ndani ya robo fainali

Martin Mwanje
1 Min Read

Mataifa ya Uhispania na Uingereza yatashiriki robo fainali ya kipute cha bara Ulaya kinachoendelea nchini Ujerumani kufuatia ushindi wa magoli 4-1 na 2-1 dhidi ya Georgia na Slovakia mtawalia.

Kwenye mechi ya kwanza, Slovakia ilipata bao kupitia Ivan Schranz dakika ya 25 huku Uingereza ikisubiri hadi muda wa majeruhi (90+5) pale Jude Bellingham alipokomboa na kulazimu muda wa ziada. Kisha Harry Kane aliongeza la pili dakika ya 91.

Katika ngarambe ya saa nne usiku, Georgia walipata bao la pekee kupitia Robin Le Normand (aliyejifunga) mnamo dakika ya 18. Uhispania walikomboa na kuongeza matatu kupitia Rodri, Fabián Ruiz, Nico Williams na Dani Olmo katika dakika za 39, 51, 75 na 83 mtawalia.

Leo Jumatatu, kiungo mtajika wa klabu ya Manchester City Kevin De Bruyne ataiongoza Ubelgiji katika pambano dhidi ya Ufaransa yake Kylian Mbappé saa moja usiku.

Kisha majira ya saa nne usiku, nahodha Christiano Ronaldo ataishika mkono Ureno kupepetana na Slovenia.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *