Uhifadhi wa Mto Nairobi: Ruto awasihi wabunge kuunga mkono juhudi

Martin Mwanje
1 Min Read

Rais William Ruto leo Jumanne amekutana na wabunge kutoka kaunti ya Nairobi kwa lengo la kutafuta uungwaji mkono wao katika juhudi za kuhifadi Mto Nairobi. 

Mkutano huo uliofanyika katika Ikulu ya Nairobi ulihudhuriwa pia na Gavana wa kaunti ya Nairobi Johnson Sakaja na Katibu katika Wizara ya Usalama wa Taifa Dkt. Raymond Omollo.

Aidha, ulihudhuriwa na wabunge ambao ni wandani wa Naibu Rais wa zamani Rigathi Gachagua akiwemo mbunge wa Embakasi Kaskazini James Gakuya.

Rigathi alikuwa mstari wa mbele kupinga ufurushaji wa wakazi wa Nairobi wanaoishi karibu na maeneo ya mito kwa ajili ya uhifadhi wa mito hiyo bila kuwatafutia makazi mbadala.

Hali hiyo wakati mmoja ilisababisha mvutanao mkali kati yake na Gavana Sakaja.

Kwenye mkutano wa leo Jumanne, Rais Ruto amewataka wabunge hao kuweka kando siasa zao na badala yake kuunga mkono juhudi za kuhifadhi Mto Nairobi.

Kwa kufanya hivyo, Rais Ruto ansema mradi huo utasaidia kubadili taswira na hadhi ya jiji la Nairobi.

Share This Article