Zoezi la kuhesabu kura lakaribia kumalizika ANC ikiongoza kwa asilimia 34.2

Dismas Otuke
1 Min Read

Shughuli ya kuhesabu kura nchini Afrika Kusini inakaribia kukamilika huku chama tawala cha ANC kikoongoza kwa asilimia 34.2 baada ya asilimia 99 ya kura kuhesabiwa.

Kulingana na tume ya uchaguzi nchini humo, IEC, chama cha Democtratic Alliance (DA) kinashikilia nafasi ya pili kwa asilimia 27.7 wakati chama cha Economic Freedom Fighters (EFF) kikishikilia nafasi ya tatu kwa asilimia 2.8%.

Chama cha uMkhonto weSizwe (MK) kimepata asilimia 9.6 ya kura zote.

Hata hivyo, ANC imehifadhi viti vingi bungeni kikizoa asilimia 52, ingawa umaarufu wake uomepungua ikilinganishwa na asilimia 61 ya viti vya ubunge kilivyozoa miaka minne iliyopita.

Chama cha DA kimezoa asilimia 21.85 ya viti vya bunge, ikiwa asilimia 4 zaidi ya mwaka 2019 huku EFF ikiwa na asilimia 13.5 ya wabunge.

Website |  + posts
Share This Article