Uganda yasaini mkataba wa mafuta na UAE

Dismas Otuke
1 Min Read

Serikali ya Uganda imesaini mkataba  na serikali ya Kifalme ya Muungano wa Milki za Kiarabu, UAE, ya ujenzi wa kiwanda chenye uwezo wa kusafisha barell 60,000 kwa siku katika wilaya ya  Hoima nchini Uganda.

Mkataba huo ulisainiwa na kutangazwa na Rais Yoweri Museveni aliyesema kuwa utasaidia kusitisha kupeleka mali ghafi za mafuta nje ya nchi kwa uchakataji.

Chini ya mkataba huo kampuni ya Alpha MBM Investments itamiliki asilimia 60 ya hisa hizo huku kampuni ya mafuta ya serikali ya Uganda ,National Oil ikimiliki asilimia 40.

Uganda sasa itajiung na mataifa yanayozalisha mafuta.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *