Uganda ilianza zoezi la Sensa ya 9 kuhesabu watu Ijumaa Mei 10 kote nchini humo huku idadi ya watu ikikadiriwa kufiki milioni 45.
Sensa ya Uganda inajiri baada ya ile ya mataifa jirani ya Rwanda,Tanzania na Kenya katika ukanda wa Afrika Mashariki .
Inakisiwa kuwa huenda taifa hilo likanakili ongezeko kubwa la watu kwenye sensa hiyo .
Zoezi hilo la sensa nchini Uganda linakabiliwa na changamoto tele zikiwemo vipakatalishi vibovu vinavyotumiwa na makarani,tofauti ya lugha ya mawasiliano,mvua na kukosa vitambulisho kwa baadhi ya raia na linatarajiwa kugharimu kima cha dola milioni 88 za Marekani.
Uganda huandaa sensa yake kila baada ya miaka 10 tangu mwaka 1911, huku idadi mpya ya watu nchini humo ikikisiwa kupanda hadi milioni 45.5 kutoka milioni 36.34 mwaka 2014.