Uganda yaanza kuuza mafuta miezi kadhaa baada ya kusitisha mkataba na Kenya

Dismas Otuke
1 Min Read

Kampuni ya kitaifa ya mafuta nchini Uganda (Unoc) imeanza kuuza bidhaa za mafuta nchini Uganda na kwa majirani Tanzania, siku chache baada ya kukatiza mkataba na Kenya.

Seriakali ya Uganda ilifanya mkataba mpya wa kuagiza mafuta moja kwa moja na kampuni ya Vitol ya Bahrain.

Kulingana na mkataba huo UNOC itaagiza mafuta kutoka Vitol kwa kipindi cha miaka mitano.

Serikalli ya Uganda ilifarakana na serikali ya Kenya kufuatia mpango mpya wa serikali wa G to G na mashirika ya mafuta ya ghuba.

TAGGED:
Share This Article