Ufaransa yazindua mtambo mpya wa kukagua mizigo ya abiria tayari kwa michezo ya Olimpiki

Dismas Otuke
1 Min Read

Maafisa wa uwanja wa ndege wa Paris Charles de Gaulle, wamezindua mtambo mpya wa kiusalama unaolenga kukagua mizigo ya abiria wakati wa makala ya 33 ya michezo ya Olimpiki itakayoandaliwa baina ya Julai na Agosti mwaka huu.

Mtambo huo wa kisasa una uwezo wa kukagua mabegi ya abiria bila haja ya kutoa nje rununu ,vifaa meme na manukatoya wasafiri kutoka kwa mikoba.

Uwanja wa ndege wa  Charles de Gaulle unatarajiwa kumudu mizigo  114,000 ya wachezaji na wanahabari watakaohudhuria michezo ya Olimpiki pamoja na mashine 47,00 itakayotumika.

Michezo ya Olimpiki itaandaliwa katiya Julai 26 na Agosti 11 mwaka huu, ikifuatwa na michezoya Olimpiki kwa walemavu itakayoandaliwa katiya Agosti 28 hadi Septemba 8 mwaka huu.

Share This Article