UDA yakataa kutimuliwa kwa Gavana Mwangaza

Dismas Otuke
1 Min Read

Chama cha United Democratic Alliance(UDA) kimelitaka bunge la kaunti ya Meru kuondoa hoja ya kumtimua Gavana  wa Meru Kawira Mwangaza .

Kwenye waraka kwa naibu kinara wa wengi katika bunge hilo Ziporah Kinya, ulioandikwa na Katibu Mkuu Cleophas Malala ,chama hicho kimelitaka bunge hilo kuahirisha hoja hiyo kwa sasa.

Malala amesema hoja hiyo huenda ikaleta mtafaruku zaidi katika chama cha UDA .

UDA badala yake imewaalika wawasilishi wa hoja hiyo katika makao makuu ya chama Jumatatu ijayo kwa kikao cha awali, kabla ya kikao kikuu Julai 25.

Gavana Mwangaza tayari amenusurika kutimuliwa ofisini mara mbili.

Baadhi ya hoja za kutaka kumtimua Gavana huyo ni pamoja na matumizi mabaya afisi.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *