UDA yajitenga na mswada wa kuongeza kipindi cha Rais

Dismas Otuke
1 Min Read

Chama cha United Democratic Alliance (UDA) kimejitenga na mswada uliopendekezwa na Seneta wa Nandi Samson Cherargei  unataoka kuongeza kipindi cha kuhudumu kwa viongozi wanaochaguliwa kutoka miaka mitano hadi saba.

Katibu Mkuu wa UDA Omar Hassan,amesema hatua hiyo inalenga kuwanyima Wakenya wengine fursa za uongozi.

Mswada huo unatarajiwa kuwasilishwa bungeni wiki ijayo.

Hassan ameutaja mswada huo kutokuwa na nia nzuri kwa taifa na na kuongeza kuwa hauakisi msimamo wa chama.

Endapo utapitishwa, muda kuhudumu wa Rais, Magavana, Maseneta, Wabunge, Wawakilishi wa Wanawake na Wadi utaongezwa kutoka miaka mitano hadi saba.

Share This Article