UDA na ODM kuwasilisha wagombea wa kumrithi Opiyo Wandayi

Dismas Otuke
1 Min Read
Rais Ruto akutana na Raila nchini Uganda.

Katika kile kinachoonekana kuwa ubabe wa kisiasa, vyama vya Orange Democratic Movement – ODM na United Democratic Alliance – UDA vimetangaza nia ya kuwasilisha wagombezi katika uchanguzi mdogo wa Ugunja. 

Uchaguzi huo mdogo unatarajiwa kuaandaliwa baada ya aliyekuwa mbunge Opiyo Wandayi kuteuliwa kuwa Waziri wa Nishati.

Uteuzi huo ulifanywa kutokana na makubaliano ya serikali jumuishi baina ya Rais William Ruto na kinara wa ODM Raila Odinga.

Katibu Mkuu wa UDA Hassan Omar, amefichua kuwa wameanza mchakato wa kumtafuta mgombea anayefaa katika kinyang’anyiro hicho.

Utakuwa mtihani wa kwanza kwa vyama hivyo viwili tangu kubuniwa kwa serikali jumuishi.

Share This Article