Uchunguzi waanzishwa kufuatia kupatikana kwa mwili wa mwanamke Embakasi

Msichana huyo anaaminika kuuawa na wanaume wawili waliokuwa wakimbaka.

Marion Bosire
1 Min Read

Maafisa wa upelelezi wameanzisha uchunguzi baada ya mwili wa mwanamke anayeaminika kuuawa kupatikana katika eneo la Embakasi, kaunti ya Nairobi.

Taarifa za mwanzo zinaashiria kwamba mwanamke huyo alinyongwa hadi akafa na wanaume wawili katika eneo la Jua Kali huko Embakasi.

Kisa hicho kilitokea usiku wa Jumatatu Machi 17, 2025 na kiliripotiwa kwa maafisa wa usalama na wakazi watatu wa eneo hilo la Jua Kali ambao walitoka nje baada ya kusikia kamsa karibu na nyumba zao usiku wa manane.

Walipiga ripoti katika kituo cha polisi cha Embakasi ambapo walielezea kwamba walipata wanaume wawili wasiojulikana wakijaribu kumbaka mwanamke huyo wa umri wa miaka 20 hivi.

Walipokaribia eneo la tukio, wanaume hao wawili walitoroka na kupotelea gizani.

Maafisa wa polisi walifika katika eneo la tukio ambapo walipata mwili wa mwanamke huyo nguo zake za ndani zikiwa zimeshushwa akiwa na alama za kunyongwa shingoni.

Eneo hilo lilishughulikiwa na maafisa hao wa usalama huku mwili ukipelekwa katika makafani ya City ambapo unasubiri kufanyiwa uchunguzi.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *