Uchumi wa Kenya ni thabiti, asema Rais Ruto

Tom Mathinji
1 Min Read
Rais wa Kenya William Ruto.

Rais William Ruto amesema uchumi wa Kenya sasa ni thabiti na unaendelea kuimarika.

Rais alisema, serikali yake imeboresha kiwango cha ubadilishanaji sarafu za kigeni na kuhakikisha kuwa kuna sarafu za kigeni za kutosha hapa nchini.

“Tumeimarisha ubadilishanaji wa sarafu za kigeni na pia tumedhibiti mfumko wa bei. Uchumi wetu sasa ni imara na unakua,” alisema Rais Ruto kupitia ukurasa wake wa X.

Kutokana na kuimarika kwa uchumi, kiongozi wa taifa alisema imani ya wawekezaji imeongezeka pamoja na mapato kutoka mataifa ya kigeni hususan katika sekta ya nishati, viwanda na maeneo maalum ya kiuchumi.

Rais aliyasema hayo leo Alhamisi Jijini Cairo,nchini Misri  baada ya kukutana na wakurugenzi wakuu wa kampuni ya  ElSewedy Electric, wakiongozwa na rais wa kampuni hiyo  Ahmed Elsewedy, pamoja na maafisa kutoka  kampuni ya Orascom Construction, wakiongozwa na mkurugenzi mkuu  Ihab Mehawed

TAGGED:
Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *