Uchaguzi wa kitaifa wa FKF kufanyika Disemba 7

Martin Mwanje
1 Min Read
Wanachama wa Bodi ya Uchaguzi ya FKF

Uchaguzi wa Kitaifa wa Shirikisho la Kandanda nchini Kenya, FKF utafanyika Disemba 7 mwaka huu. 

Uchaguzi huo katika ngazi ya kaunti utafanyika kesho Alhamisi, Novemba 14, 2024.

Hii ni baada ya mahakama kuondoa maagizo yaliyokuwa yamezuia kuandaliwa kwa uchaguzi huo.

Kwenye taarifam, mwenyekiti wa Bodi ya Uchaguzi ya FKF Hesbon Owilla na Katibu wa Uchaguzi wa FKF Marceline Sande wamesisitiza kujitolea kwa bodi hiyo kusimamia uchaguzi huo kwa njia ya haki na uwazi.

Wakati wa uzinduzi wa Bodi ya Uchaguzi ya FKF katikati ya mwezi Septemba mwaka huu, Owilla aliahidi kufanya kazi na timu huru itakayohakikisha uadilifu wa uchaguzi huo.

TAGGED:
Share This Article