Chama cha Authenticity and Modernity (PAM) kimetwaa viti vingi kwenye uchaguzi wa ubunge ulioandaliwa jana Jumatano nchini Morocco.
Wizara ya Mambo ya Ndani imetangaza kuwa PAM ilizoa viti 97, kile cha National Rally of Independents (RNI) kimepata wabunge 66 huku kile cha Istiqlal kikijinyakulia wabunge 65.
Chama cha Justice and Development Party (PJD) kilichukua nafasi ya nne kwa jumla ya wabunge 54.
Uchaguzi huo ulishuhudia idadai ndogo ya wapiga kura ikiwa asilimia 38 pekee, ikilinganishwa na asilimia 50 ya wapiga kura waliojitokeza mwaka 2021.
Wapiga kura milioni 15.8 walijisajili kwa uchaguzi wa mwaka huu ulioshirikisha vyama 28, ingawa ni wapiga kura milioni 6 pekee waliojitokeza kupiga kura.
Jumla ya wagombeaji 1,847 walijitosa kuwania viti mbalimbali katika uchaguzi huo uliowashirikisha wanawake 2,659, ikiwa ni asilimia 37 ya wawaniaji wote.