Sudan Kusini imeahirisha uchaguzi mkuu wa kwanza ulioratibiwa kuandaliwa tarehe 22 mwezi ujao hadi Februari 11 mwaka ujao.
Hatua hiyo ina maana kuwa Sudan Kusini itasubiri kwa muda mrefu zaidi kabla ya kuandaa uchaguzi tangu ijinyakulie uhuru mwaka 2011.
Tume ya uchaguzi nchini Sudan Kusini ilitangaza kuahirisha uchaguzi huo huku ikisema kuwa matokeo rasmi yatatangazwa ifikiapo Februari 15 mwaka ujao.
Yamkini uchaguzi huo umeahirishwa kutokana na uhasama wa kisiasa na kikabila unaoshuhudiwa nchini humo .
Majeshi waaminifu wa Rais Salva Kiir na wafuasi wa Makamu Rais wa zamani Riek Machar aliyewekwa kwa kifungo cha nyumbani tangu mwaka 2025 wamekuwa wakikabiliana kwa muda sasa nchini humo.