Bafana Bafana watua Kenya kuikabili Harambee Stars

Dismas Otuke
1 Min Read

Timu ya taifa ya Afrika Kusini imewasili Nairobi Jumamosi Adhuhuri tayari kwa mechi ya kufuzu kwa fainali za mwala ujao za AFCON  dhidi Kenya wiki ijayo.

Bafana Bafana imetua Nairobi leo baada ya kulazimishwa kwenda sare ya mabao 2 na Harambee Stars Ijumaa usiku mjini Johannesburg,katika mkumbo wa kwanza wa mechi hiyo ya kundi D.

Kenya itawaalika Afrika Kusini Jumanne jioni katika uwanja wa kitaifa wa Nyayo huku wakisaka ushindi wa kwanza kundini wakiwa na alama mbili pekee.

Afrika Kusini wanaongoza kwa pointi 7 ,moja zaidi ya Guinea walio katika nafasi ya pili huku Kenya wakishikilia nafasi ya tatu.

 

Share This Article