Uchaguzi Mkuu wa DRC wagubikwa na vurugu

Dismas Otuke
1 Min Read

Uchaguzi mkuu ulioandaliwa Jumatano katika Jamhuri ya Kidemkokrasia ya Congo, DRC uligubikwa na vurumai, maandamano na madai ya wizi wa kura.

Katika baadhi ya vituo vya kupigia kura, zoezi hilo lilicheleweshwa kuanza huku vingine vikikosa kufunguliwa.

Uchaguzi huo uliongezwa muda hadi siku ya Alhamisi katika sehemu ambazo haukuandaliwa Jumatano.

Wawaniaji wanne wa upinzani wanataka kufutiliwa mbali kwa uchaguzi huo.

Rais Félix Tshisekefi anawania muhula wa pili huku akipambana na wawaniaji wengine 18.

Taifa hilo lina idadi ya wapiga kura milioni 44 waliojisajili.

Share This Article