Tume huru ya uchaguzi na uratibu wa mipaka (IEBC) imetangaza kuwa uchaguzi mdogo wa eneo bunge la Emurua Dikirr utaandaliwa Mei 14 mwaka huu.
IEBC imewataka wote wanaonuia kuwania kiti hicho kuwasilisha karatasi zao kabla au kufikia tarehe 7 mwezi ujao.
Mwenyekiti wa IEBC Erastus Ethekon amemteua Caleb Siriba Gekendo, kuwa msimamizi wa uchaguzi mdogo wa Emurua Dikirr akisaidiwa na Sylvia Jepchumba.
Ethokon ametangaza kuwa IEBC inahitaji bajeti ya shilingi milioni 59.38, kuandaa uchaguzi mdogo wa Emurua Dikirr.
Kiti hicho kiliachwa wazi kufuatia kuaga dunia kwa Mbunge Johanna Ng’eno, kupitia ajali ya ndege ya Februari 28 mwaka huu.