Ubalozi wa Marekani nchini Canada washambuliwa

Shambulizi hili linatokea huku polisi wa Norway wakichunguza mlipuko uliotokea nje ya ubalozi wa Marekani huko Oslo siku ya Jumapili.

Tom Mathinji
1 Min Read
Ubalozi wa Marekani nchini Canada washambuliwa.

Taarifa na BBC.

Maafisa wa polisi nchini Canada wachunguza shambulizi lililotekelezwa dhidi ya ubalozi wa Marekani na watu wasiojulikana.

Washukiwa hao wanadaiwa kushambulia ubalozi wa Marekani huko Toronto kwa risasi,katika kile ambacho maafisa wamekielezea kuwa “tukio la usalama wa taifa”, huku polisi wakijitahidi kubaini chanzo cha shambulio hilo.

Mamlaka ilisema shambulizi hilo lilitokea mapema Jumanne asubuhi, ambapo maafisa walipata maganda ya risasi kwenye eneo la tukio na jengo lilikuwa limeshambuliwa, alisema Frank Barredo, naibu mkuu wa Polisi wa Toronto.

Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani ilisema inafahamu kuhusu tukio hilo na inafuatilia kwa karibu hali hiyo kwa kushirikiana na vyombo vya sheria vya eneo hilo.

Shambulizi hili linatokea huku polisi wa Norway wakichunguza mlipuko uliotokea nje ya ubalozi wa Marekani huko Oslo siku ya Jumapili.

Share This Article