Makala ya 20 ya tuzo za kila mwaka za wanamichezo bora nchini Kenya maarufu kama SOYA yataandaliwa Ijumaa usiku katika ukumbi wa mikutano ya kimataifa wa KICC.
Tuzo hizo ziliasisiwa mwaka 2003 na Rais wa kamati ya Olimpiki nchini Kenya NOCK Dkt. Paul Tergat kwa madhumuni ya kuwatambua na kuwatuza wanamichezo wanaofanya vyema kila mwaka.
Bingwa mara mbili wa Olimpiki katika mita 10,000 na bingwa mara 4 wa dunia Haile Gebreselasie kutoka Ethiopia atakuwa mgeni wa heshima wa hafla ya mwaka huu ikisadifiana na makala ya kwanza miaka 20 iliyopita alipoalikwa kuwa mgeni mstahiki.
Vitengo vitakavyowaniwa katika tuzo za mwaka huu ni mwanaspoti bora wa jumla, mwanaspoti bora wa kiume na kike, mwanaspoti bora wa kiume na kike kwa walemavu, timu bora ya mwaka kwa wanume na wanawake na shule bora ya mwaka kwa wasichana na wavulana.
Mabingwa wa Olimpiki Faith Kipyegon na Eliud Kipchoge watatuzwa kama wanaspoti bora mwaka jana.