Tuzo za CAF za wanasoka bora kuandaliwa Marrakech Disemba 11

Dismas Otuke
1 Min Read

Hafla ya kuwatuza wanasoka bora barani Afrika itaandaliwa katika jiji la kitalii la Marrakech nchini Morocco Disemba 11.

Sherehe hizo zitaandaliwa nchini Morocco
kwa mwaka wa pili na zitashuhudia kutambuliwa kwa wachezaji bora katika vitengo mbalimbali kama vile mchezaji bora
kwa wanaume na wanawake, kipa bora, mchezaji bora anayecheza soka barani Afrika na wachezaji chipukizi bora.

Mshambulizi wa Senegal Sadio Mane alituzwa mwanandinga bora mwaka uliopita baada ya kunyakua kombe la Afrika na Teranga Lions.

Share This Article