Makala ya mwaka huu ya tuzo za wachezaji bora Afrika yataandaliwa leo usiku mjini Marrakech,Morocco .
Kutakwua na jumla ya vitengo 15 vya tuzo hizo zikiwemo mchezaji bora kwa wanaume na wanawake,kocha bora,klabu bora kwa wanaume na wanawake,kipa bora na mcjezaji bora kwa wale wanaosakata soka humu barani kwa wanaume na wanawake,miongoni mwa vitengo vinginevyo.
Itakuwa mwaka wa pili mtawalia kwa tuzo hizo kuandaliwa Marrakech,Morocco baada ya mwaka jana.
Wachezaji watano wa mwisho wanaowania tuzo ya wanaume ni: Ronwen Williams kutoka South Africa, Simon Adingra wa Cote d’Ivoire, Serhou Guirassy wa Guinea, Achraf Hakimi wa Morocco na Ademola Lookman wa Nigeria.
Sadio Mane wa Senegal alishinda tuzo hiyo mwaka 2022, huku Victor Osimhen kutoka Nigeria akitawazwa mshindi wa mwaka jana.
Tuzo ya wanawake inawaniwa na:Sanâa Mssoudy wa Morocco, Chiamaka Nnadozie kutoka Nigeria na Barbra Banda wa Zambia.
Nahodha wa zamani wa Harambee Stars Victor Wanyama atahudhuria hafla ya leo huku msanii wa Bongo Diamond Platinumz akitarajiwa kutumbuiza.