Tuwei achaguliwa makamu Rais wa Shirikisho la Riadha Ulimwenguni

Dismas Otuke
1 Min Read

Rais wa Shirikisho la Riadha Kenya Jenerali mstaafu Jackson Tuwei, amechaguliwa kuwa mmoja wa makamu Rais wa Shirikisho la Riadha Ulimwenguni kwenye uchaguzi ulioandaliwa wakati wa kongamano kuu la 54  jijini Budapest nchini Hungary mapema Alhamisi.

Tuwei alizoa kura 104 nyuma ya mwanariadha wa Colombia Ximena Restrepo aliyeongoza kwa kura 154. Mwanariadha mstaafu wa Uhispania Raul Chapado aliyefuata katika nafasi ya pili kwa kura 119 na mwanariadha wa zamani wa mbio za masafa mafupi wa India Adille Sumariwalla aliyepata kura 115.

Tuwei pia ni makamu Rais wa Shirikisho la Riadha Afrika na Rais wa Muungano wa Mashirikisho ya Riadha Afrika Mashariki.

Rais wa Shirikisho la Riadha Duniani Sebastien Coe amechaguliwa bila kupingwa kuhudumu kwa kipindi kingine cha miaka minne.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *