‘Tutakomesha utekaji nyara,’ asema Rais Ruto

Dismas Otuke
2 Min Read
Rais Ruto na Raila wakiwa katika kaunti ya Homa Bay Ijumaa kuhudhuria fainali ya Kombe la Gavana wa kaunti hiyo.

Rais William Ruto ameahidi kuwa serikali yake itakomesha utekaji nyara wa raia ambao umekuwa ukiongezeka katika siku za hivi karibuni na kuhakikisha usalama wa vijana wa taifa hili.

Akizungumza katika kaunti ya Homa Bay, Ruto aliwataka vijana kuzingatia maadili na kuwa na nidhamu, huku akitoa changamoto kwa wazazi kutoa makuzi bora kwa wanao.

“Maneno ya abductions tutakomesha ndiyo vijana wa Kenya waweze kuishi kwa amani na vile vile wawe na nidhamu and wawe wangwana,” alisema Ruto

Ilikuwa mara ya kwanza kwa Rais kuzungumzia idadi ya vijana wanaotoweka humu nchini katika hali tatanishi, huku matamshi yake yakikinzana na yale ya  idara ya polisi iliyokana kuhusika katika utekaji nyara huo.

Rais Ruto alisema hayo jana alipohudhuria fainali ya soka ya kombe la Gavana wa Homa Bay Gladys Wanga almaarufu Genowa Governor’s Cup katika uwanja wa Raila Odinga.

Fainali hiyo ilihudhuriwa na Raila Odinga, Gavana Wanga, Katibu wa Usalama wa Ndani Raymond Omollo, kiongozi wa wengi katika bunge la kitaifa Kimani Ichung’wah, Waziri wa Nishati Opiyo Wandayi na kiongozi wa walio wachache katika bunge la kitaifa Junet Mohamed miongoni mwa vongozi wengine.

Tume ya kutetea haki za kibinadamu, KNCHR ilisema juzi kuwa jumla ya watu 82 wametekwa nyara nchini tangu mwezi Juni huku 29 wakiwa hawajapatikana kufikia leo.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *