Tusker wakabwa koo,Gor wateleza nyumbani

Gor wana mlima wa kukwea  ambapo watahitaji ushindi wa mabao 3-2 ugenini nchini Misri mwishoni mwa juma hili, ili kufuzu kwa raundi ya pili.

Dismas Otuke
1 Min Read

Tusker FC walirejea kwa mashindano ya Afrika kwa mara ya kwanza baada ya muda mrefu, kwa njia ya kipekee walipolazimisha sare ya mabao 2 dhidi ya Madani FC ya Sudan,Jumapili jioni katika mechi ya raundi ya kwanza mkumbo wa kwanza kuwania Kombe la Shirikisho.

Tusker watawaalika Madani mwishoni mwa juma hili huku wakihitaji sare tasa, ili kusonga mbele katika kombe hilo.

Wakati uo huo mbingwa wa ligi ya Kenya Gor Mahia, walisalimu amri na kuambulia kichapo cha magoli  mawili bila jibu kutoka kwa mabingwa wa Misri Pyramids FC katika duru ya kwanza ya raundi ya kwanza iliyosakatwa Jumapili alasiri katika uwanja wa Nyayo.

Gor wana mlima wa kukwea  ambapo watahitaji ushindi wa mabao 3-2 ugenini nchini Misri mwishoni mwa juma hili, ili kufuzu kwa raundi ya pili.

Huku hayo yakijiri Gor wametangaza kukusanya shilingi milioni 3.8 kutoka na uuzaji tiketi za mechi hiyo.

Kulingana na taariufa kupitia mitandao ya kijamii ya klabu hiyo ,jumla ya tiketi 11,282 ziliuzwa.

Share This Article