Rais William Ruto amearai Wakenya kupanda miti kwa wingi ili kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi.
Ruto alisema haya alipoongza upanzi wa miti katika msitu wa Karua forest eneo bunge la Maragua , akielezea imani yake ya jumla ya miti milioni 200 kupandwa kufikia mwisho wa Ijumaa.
Rais amekariri wito na ajenda ya serikali kupanda miche ya miti bilioni 15, ili kuongeza utandu wa misitu kutoka asilimia 12 hadi 30 ifikiapo mwaka 2032.
Siku ya Ijumaa Mei 10 ilitangazwa kuwa siku kuu ya kitaifa kwa upanzi wa miti.