Tunajivunia mawazo ya hekima ya Odinga, asema Rais Ruto

Tom Mathinji
1 Min Read
Rais William Ruto.

Rais William Ruto amesema serikali inajivunia mawazo yenye hekima, maono na maoni yaliyotolewa na aliyekuwa Waziri Mkuu Raila Odinga wakati wa hotuba yake kwenye mkutano wa tatu wa kitaifa wa Baraza la Mawaziri ulioandaliwa Karen,Nairobi.

Kupitia ukurasa wake wa X leo Ijumaa, Rais Ruto alisema wito wa Raila kwa viongozi waangazie yaliyo mema baadala ya kutaka umaarufu, unaambatana na malengo ya serikali yake.

Alisema serikali imepata mafunzo mengi kutoka kwa Raila kuhusu utekelezaji wa miundombinu ya kitaifa, ikiwemo mradi wa ujenzi wa nyumba za gharama nafuu,ujenzi wa masoko ya mazao ya kilimo na upanuzi wa viwanja  vya ndege miongoni mwa miradi mingine.

“Tumejifunza kutoka kwa mawazo ya Odinga kuhusu mipango ya kitaifa ya miundomsingi, kama vile ujenzi wa nyumba za bei nafuu, masoko ya bidhaa za kilimo, upanuzi wa viwanja vya ndege, miongoni mwa mingine,” alisema kiongozi wa taifa.

Raila pia alijadilia jukumu muhimu la teknolojia katia kuleta mabadiliko humu nchini,ikiwemo akili unde na akaipongeza serikali kwa kuendeleza kutekeleza mpango wake wa kutoa huduma zake kidijitali.

Website |  + posts
Share This Article