Tume ya utumishi wa umma yatangaza nafasi za kazi 532

Dismas Otuke
1 Min Read

Tume ya utimishi wa umma PSC imetangaza nafasi za kazi 532, katika idara mbali mbali za serikali kote nchini.

Kulingana na tangazo kwa umma tume ya PSC imetangaza nafasi moja ya katibu katika idara ya utangazaji na mawasiliano, naafsi 23 katika huduma ya matibabu nchini,nafasi 177 katika idara ya usalama wa ndani na usimamizi wa kitaifa na maafisa wengine 106 katika wizara ya Ulinzi.

Nafasi nyinginezo zilizotangazwa ni 19 katika katika idara ya vyama vya ushirika,60 katika mradi wa mabadiliko ya tabianchi, na nyingine 144 katika wizara ya Leba na maendeleo.

Wanaopania kutuma maombi wanashauriwa kusakura tovuti ya website www.publicservice.go.ke,au ile ya ww.psckjobs.go.ke.

TAGGED:
Share This Article