Tume ya Rais kuhusu Mabadiliko katika Vikosi vya Usalama nchini iliyoongozwa na Jaji Mkuu mstaafu David Maraga, imefuchua uozo mkubwa katika vikosi vitatu vikuu nchini.
Kulingana na ripoti ya tume hiyo, kuna ufisadi mkubwa katika idara ya magereza, polisi wa kitaifa na idara ya huduma ya taifa kwa vijana, NYS.
Viwango vya juu vya upokeaji hongo hutokea hususan wakati wa kuwaajiri makurutu wakitoa rushwa ya hadi shilingi elfu 600 ili kununua nafasi za kuajiriwa.
Maraga ameongeza kuwa baadhi ya mambo yanayoathiri vikosi vya usalama ni mapendeleo, ukabila na urafiki kazini.
Akipokea ripoti hiyo jana Alhamisi, Rais William Ruto aliagiza kutekelezwa kwa mapendekezo yake mara moja.