Tume ya Maadili na Kupambana na Ufisadi, EACC imerejesha shamba la ekari tano na nyumba 20 zilizokuwa zimenyakuliwa kwa wizi.
EACC imesema shamba la Wizara ya Nyumba na Maenedeleo ya Miji la ekari 5, lilikuwa limevamiwa na wastawishaji wa kibinafsi katika kaunti ya Nakuru.
Shamba hilo la serikali lilikuwa limetengewa upanuzi wa barabra, kilimo na ujenzi wa nyumba za serikali.
Ilibainika baadaye kuwa lilikuwa limenyakuliwa kwa njia za kilaghai.