Tume ya kitaifa ya huduma kwa polisi yabatilisha upandishaji vyeo wa hivi maajuzi

Dismas Otuke
1 Min Read

Tume ya kitaifa ya huduma kwa polisi (NPSC) imebatilisha upandishaji vyeo kwa maafisa wa polisi, uliotekelezwa maajuzi na kaimu Inspekta Mkuu wa Polisi Gilbert Masengeli.

Menyekiti wa tume hiyo Eliud Kinuthia amemwagiza Masengeli kusitisha upandishaji vyeo hadi pale Kamishna mpya wa Polisi atakapoteuliwa.

Hii inafuatia hatua ya maajuzi ambapo polisi 1,957 wakiwemo wanaume 1,8709 na wanawake 87 kati ya umri wa miaka 53-59, ambao hawakuwa na rekodi yoyote ya utovu wa nidhamu waliidhinishwa kupandishwa vyeo na tume hiyo .

Upandishaji vyeo huo umebatilishwa kufuatia malalamishi kutoka kwa maafisa wengine waliosema wamekawia katika wadhfa mmoja kwa muda mrefu bila kupandishwa vyeo.

Hali ya kuwapandisha vyeo polisi hao ni ilikuwa ya kuwamotisha kabla ya kustaafu.

Share This Article