Tuju ashtakiwa kwa kutoa habari za kupotosha

Tom Mathinji
1 Min Read
Waziri wa zamani Raphael Tuju aachiliwa kwa dhamana ya shilingi 100,000.

Waziri wa zamani Raphael Tuju, amefunguliwa mashtaka katika mahakama ya Kbra, kwa kutoa habari za kupotosha kwa afisa wa polisi.

Mashtaka hayo yanahusishwa na ripoti iliyotolewa Machi 1,2026 katika kituo cha polisi cha Karen, ambapo Tuju alidai alikuwa ametekwa nyara.

Akifika mbele ya Hakimu Mkuu Mwandamizi Stella Atambo, Tuju alikanusha mashtaka hayo.

Kupitia wakili wake Edward Oonge, Tuju aliomba kuachiliwa kwa dhamana, akidai kuwa mashtaka hayo hayana uzito wa kumsababisha aendelee kuzuiliwa.

Mahakama hiyo ilimwachilia Tuju kwa dhamana ya kibinafsi ya shilingi 100,000, na kuagiza kuachiliwa kwa gari lake lililokuwa likizuiliwa katika kituo cha polisi cha Karen.

Kesi hiyo itatajwa Aprili 15,2026.

Kesi hiyo inatokana na uchunguzi uliotekelezwa na maafisa wa Idara ya Upelelezi wa Makosa ya Jina (DCI), uliobainisha kuwa Tuju alisalia nyumbani kwake  katika kipindi alichodai alikuwa ametekwa nyara.

TAGGED:
Share This Article