TSC yapuuza mapendekezo ya tume ya Rais kuhusu elimu

Dismas Otuke
1 Min Read

Tume ya kuwaajiri Walimu TSC imepuuzilia mbali baadhi ya mapendekezo ya tume ya Rais ya elimu, ambayo inapendekeza wizara ya elimu kusimamia mafunzo na kupandishwa vyeo kwa walimu.

TSC imekuwa ikisimamia mafunzo ya walimu walio kazini na kupandisha vyeo na kulinagana na afisa mkuu mtendaji Nancy Macharia, utakuwa ukiukaji wa sheria.

Tume ya Rais kuhusu elimu inayoongozwa na profesa Raphael Munavu ilitoa mapendekezo kadhaa ya kubadilisha mfumo wa elimu nchini.

Hata TSC imelalama kuwa tume hiyo haikuzingatia maoni yake yaliyotolewa katika kaunti ya Mombasa wakati wa kuu da ripoti ya mwisho.

TAGGED:
Share This Article