TSC: Walimu Kenya wamefanya kazi maridhawa

Martin Mwanje
1 Min Read

Walimu nchini Kenya wamemakinika mno katika utekelezaji wa majukumu yao. 

Hayo yamesemwa na Tume ya Kuwaajiri Walimu, TSC wakati wa maadhimisho ya Siku ya Walimu Duniani yanayofanyika leo Alhamisi.

Afisa Mtendaji wa tume hiyo Nancy Macharia ametaja wajibu muhimu uliotekelezwa na walimu kurejesha ratiba ya kalenda ya masomo; uwezeshaji wa mpito wa wanafunzi wa Gredi ya 6 hadi ile ya 7; na kushiriki kwao katika mafunzo ya utekelezaji wa mfumo wa umilisi, CBC kuwa sababu tosha za kuwasherehekea walimu kila pembe ya nchi.

Macharia anasema sababu zingine zisizopaswa kusahaulika ni mapitio yaliyofanikiwa ya Mkataba wa Makubaliano ya Pamoja, CBA wa mwaka 2021-2025 na usimamiaji wa mitihani ya kitaifa ya mwaka 2023.

Ulimwengu huungana kuadhimisha Siku ya Walimu Duniani kila Oktoba 5 ambapo mchango wa walimu katika sekta ya elimu hutambuliwa na kuenziwa.

Siku hiyo ilitengwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni, UNESCO mnamo mwaka wa 1994 ambapo maadhimisho ya kwanza yaliandaliwa.

Share This Article