TSC kukutana na vyama vya walimu kujadili nyongeza ya mishahara

Dismas Otuke
1 Min Read

Tume ya kuwaajiri walimu TSC inatarajiwa kukutana na vyama vya walimu wiki hii kujadili kuhusu nyongeza mpya ya mishahara.

Vyama vya walimu vinatarajiwa kufanyia mabadiliko nyongoeza ya mishahara iliyoafikia kati ya mwaka 2021 hadi 2025(CBA), iliyotiwa saini Julai mwaka 2021 kutokana na makali ya ugonjwa wa Uviko 19 kwa uchumi wa nchi.

Mkataba wa makubaliano ya pamoja kuhusu mishahara ya mwaka 2021 ulitiwa saini na vyama vitatu vikuu vya walimu KNUT,KUPPET na KUSNET.

Kikao hicho kimeratibwa kuandaliwa siku ya Jumanne katika chuo cha kutoa mafunzo kwa wafanyikazi wa serikali (Kenya School of Government).

TSC imewaalika viongozi wa vyama vya walimu kufuatia hatua ya tume ya kusimamia mishahara SRC kutangaza nyongeza ya kati ya asilimia 7 na 10 kwa watumishi wa umma kwa kipindi cha miaka miwili ijayo.

Website |  + posts
Share This Article