Rais mteule wa Marekani Donald Trump huenda akaiondoa nchini hiyo kuwa mwanachama wa Shirika la Afya Dunini, WHO, punde atakapoapishwa mwezi ujao.
Wanachama wa jopo la mpito wa uongozi wa Rais Trump yamkini wameanza kuweka mikakati ya Marekani kujiondoa kuwa mwanachama wa WHO.
Hii ni baada ya Trump kulishutumu shirika hilo kwa kushindwa kuiadhibu China kutokana na kile alichokitaja kuwa kusababisha virusi vya Covid-19 kimakusudi.
Trump amesema hela ambazo Marekani imekuwa ikilipa WHO huenda zikaelekezwa kwa miradi mingine ya kusaidia jamii.
Trump alikuwa ameweka mpangilio wa kuiondoa Marekani kwa WHO mwaka 2020, akiwa Rais lakini mchakato huo ukasitishwa miezi sita baadaye baada ya kushindwa na Rais wa sasa Joe Biden a,iyefutilia mbali mpango huo.
Endapo atafanikiwa, huenda mashirika ya kimataifa kama WHO ikaitenga Marekani katika juhudi za kukabiliana na majanga ya kimataifa kama magonjwa mapya.