TP Mazembe watwaa taji ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa vidosho

Dismas Otuke
1 Min Read

TP Mazembe ya Jamhuri ya Demokrasia ya Congo ndio washindi wa makala ya nne ya taji la Ligi ya Mabingwa Afrika .

Mazembe walitawazwa mabingwa baada ya kuwalaza wenyeji ASFAR ya Morocco, bao moja kwa bila katika fainali iliyosakatwa katika uwanja wa Ben Ahmed El Abdi mjni El Jadida.

Bao la ushindi lilipachikwa wavuni kunako dakika ya 10 kupitia kwa Marlene Kasaj na likadumu hadi kipenga cha mwisho.

Kufuatia ushindi huo Mazembe walituzwa kombe pamoja dola laki sita, huku ASFAR wakitia mkobani dola laki nne.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *