Tonto Dikeh asema ameokoka

Marion Bosire
1 Min Read

Mwigizaji wa filamu za Nollywood nchini Nigeria ambaye pia ni mwanasiasa, Tonto Dikeh, amezua gumzo kubwa kwenye mitandao ya kijamii baada ya kufichua kwamba amekabidhi maisha yake yote kwa Yesu Kristo.

Mwigizaji huyo, ambaye hivi karibuni alihudhuria hafla ya Kikristo nchini Ghana, alieleza kuwa hatamani tena mambo ya dunia na sasa amejiweka wakfu kabisa kwa imani yake.

Akiweka wazi kujitolea kwake upya, Tonto aliandika, “YESU HUYU NILIYEMPATA, nimemshika kwa kiuno. Hakuna kingine tena duniani kwa ajili yangu. Yesu, ukinibariki au usininibariki, nitasimama, usiponibariki nipo hapa.”

Alifuatisha chapisho hilo na video kadhaa zikimuonyesha akiwa katika ibada ya kina wakati wa mkutano wa kiroho nchini Ghana, alionyesha pia mabadiliko makubwa na kujitolea kwake kwa imani ya Kikristo.

Aliongeza kusema, Mungu yupo kweli kila mahali; uwepo Wake ulikuwa dhahiri — mpole lakini wenye nguvu, ukinivuta zaidi katika kujisalimisha Kwake. Wakati huo, hakuna kingine kilichokuwa na maana zaidi ya Yeye.

Haikuhusu mahali au mtu, bali ilikuwa ni Mungu akijidhihirisha upya na kunikumbusha kuwa bado yupo karibu, bado anazungumza, bado anabadilisha mioyo. Niliondoka nikiwa na hofu mpya ya utukufu Wake na shauku kubwa zaidi ya kumjua kwa undani.”

Website |  + posts
Share This Article