Mwigizaji na mwanasiasa wa Nigeria Tonto Dikeh huenda akapunguza makalio aliyoongezewa hospitalini. Hii ni baada ya kushika nafasi ya pili kwenye mashindano ya mbio kati ya wazazi katika shule ya mwanawe.
Dikeh ambaye alikuwa akiwania unaibu gavana kwenye uchaguzi uliopita nchini Nigeria alichapisha video akishiriki shindano hilo akisema kwamba uzito wa makalio hayo ndio ulimfanya awe nambari mbili na sio nambari moja.
Alitaja kliniki ambapo alipokea huduma ya kuongeza makalio akisema itabidi wapunguze kwa sababu ni mazito mno.
Mama huyo wa mtoto mmoja alisema kwamba yeye ni mama ambaye anatekeleza jukumu la mzazi kwa umakinifu mkubwa ndiposa anahudhuria mashindano kama hayo katika shule anayosomea mwanawe.
Katika shindano hilo mwaka jana Tonto aliibuka mshindi tofauti na mwaka huu na tayari amempongeza mama aliyeibuka mshindi mwaka huu.