Tom Green atangaza uchumba na Amanda

Mwigizaji huyo alichapisha kwenye ukurasa wake wa Instagram ambapo alitangaza kwamba ataoa mpenzi wake, aitwaye Amanda.

Marion Bosire
1 Min Read

Mchekeshaji Tom Green yuko tayari kujaribu ndoa tena, zaidi ya miongo miwili baada ya kutengana na Drew Barrymore kama vile alivyotangaza hivi karibuni kuhusiana na uhusiano wake mpya.

Mwigizaji huyo alichapisha kwenye ukurasa wake wa Instagram ambapo alitangaza kwamba ataoa mpenzi wake, aitwaye Amanda.

Aliandika, “Habari kubwa! Amanda na mimi tumekuwa wapenzi! Mimi ni mwanaume mwenye bahati duniani. Nakupenda Amanda. Krismasi njema na furaha kutoka kwetu kwenu sote!”

Tom pia alichapisha picha kadhaa za uchumba wao ambazo zilionyesha kwa karibu pete nzuri ya almasi aliyomvisha mpenzi wake.

Hakuna mengi yanayojulikana kuhusu uhusiano wa Tom na Amanda, kwani alitangaza rasmi uhusiano wao kwenye Instagram mwezi Juni.

Hata hivyo, wawili hao wanavyoonekana kuwa na upendo mkubwa kwa kila mmoja, wakipeana mabusu kwenye picha moja baada ya uchumba wao.

Hii haitakuwa mara ya kwanza kwa Tom kuoa, alikuwa amemwoa mwigizaji Drew Barrymore Julai 2001, ndoa iliyodumu muda mfupi.

Tom aliwasilisha kesi ya talaka mwezi Disemba wa mwaka huo huo.

Talaka yao ilikamilishwa Oktoba 2002 na wawili hao hawakukutana tena hadi Tom alipoonekana kwenye kipindi cha mazungumzo cha Drew mwaka 2021.

Wakati huo, wawili hao walisema bado wanapendana lakini hawakurejelea uhusiano wao wa kimapenzi.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *