Tom Alila ajitosa kuwania Urais wa FKF

Dismas Otuke
1 Min Read

Aliyekuwa mwanachama wa shirikisho la soka nchini kutoka Nyanza Tom Alila ametangaza kuwania Urais katika uchaguzi wa Disemba 7 mwaka huu.

Alila,amezindua kampeini yake Jumanne jijini Nairobi huku akiangazia ajenda za kukuza soka kutoka mashinani,kukuza soka ya wanawake na kuboresha maslahi ya wachezaji.

“Nitahakikisha kuna uwazi,uwajibikaji na upatikanaji wa huduma kwa kila mmoja anayehitaji.Tutaandaa ripoti ya fedha ambayo itachunguzwa na umma na kumshirikisha kila mdau katika kufanya maamuzi.

Soka ya mashinani ndio nguzo ya soka yetu ,lazima tuekeze kwa miradi ya soka ya chipukizi Gtukipanda juu.”akasema Alila

Mfanyabishara huyo amesisitiza kuwa soka inaweza kubadilisha maisha ya mamilioni ya watu kwa njia moja au nyingine endapo itapata usimamizi bora, na akichaguliwa atawashirikisha wadau wote katika usimamizi wa soka na pia kubuni shirika huru litakaloendesha ligi zote kinyume na sasa ambapo Ligi hizo zinasimamiwa na kuendeshwa na shirikisho.

Alila ameahidi kuweka mpangilio bora wa kuendesha ligi ya wanwake na kuongeza kiwango cha pesa kwa usimamizi wa soka ya wanawake amoja na kuimarisha maslahi ya wachezaji.

Alila ni mwaniaji wa pili kutangaza azma ya kuwania kiti hicho baada ya Afisa Mkuu wa Extreme Sports Hussein Mohammed aliyezindua kampeini yake mwezi uliopita.

Waaniaji wote watatathminiwa na kuidhishwa na bodi ya uchaguzi.

Website |  + posts
Share This Article