Tina Knowles ajibu wakosoaji wa tumbuizo la binti yake Beyoncé

Beyonce alikuwa mtumbuizaji mkuu wa pumziko la katikati ya mchezo wa soka wa timu za Houston Texans-na Baltimore Ravens nyumbani kwao huko Houston lakini wapo ambao hawakuridhishwa na kazi yake.

Marion Bosire
1 Min Read

Mamake mwanamuziki Beyonce Tina Knowles amejibu wakosoaji wa tumbuizo lake la katikati ya mchezo wa soka siku kuu ya Krismasi.

Beyonce alikuwa mtumbuizaji mkuu wa pumziko la katikati ya mchezo wa soka wa timu za Houston Texans-na Baltimore Ravens nyumbani kwao huko Houston lakini wapo ambao hawakuridhishwa na kazi yake.

Knowles alitumia akaunti yake ya Instagram kujibu wakosoaji hao akisema, “Inanishangaza kuona kwamba unatumia muda wako siku ya Krismasi kutazama tumbuizo la mtu unayemchukia na unayedhani hana talanta ili uende ukamseme vibaya.”

Mama huyo aliendelea kusema kwamba wakosoaji wanadhihirisha kwamba wanampenda Beyoncé zaidi lakini hawawezi kukubali hilo waziwazi.

Onyesho la Beyonce hata hivyo lilifana kulingana na wengi ripoti zikionyesha kwamba zaidi ya watu milioni 27 walitazama tumbuizo hilo kwenye Netflix.

MMoja wa wakosoaji wakuu wa tumbuizo la Beyonce ni Dave Portnoy mfanyabiashara ambaye ni maarufu mitandaoni nchini Marekani.

Kulingana na Portnoy Beyonce alipotea kimuziki tangu alipoondoka kwenye kundi la Destiny’s Child mwaka 2006 ambako alikuwa akiimba pamoja na Kelly Rowland na Michelle Williams, kabla ya kuanza kuimba peke yake.

Knowles anashauri wakosoaji hao kujishughulisha na mambo mengine kama kutizama filamu za vibonzo wakati wa mapumziko unapowadia na kurejelea kutazama mchezo baada ya tumbuizo.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *