Timu ya taifa ya Kenya -Harambee Stars, itachuana leo usiku na Gambia, katika mechi ya mzunguko wa tano kundini F, kufuzu kwa fainali za Kombe la Dunia mwaka ujao.
Mchuano huo utasakatwa katika kiwara cha Alllasane Quatarra nchini Ivory Coast, kuanzia saa nne usiku.
Kenya haina budi kuapata ushindi ili kuweka hai matumaini ya kufuzu, ikikalia nafasi ya nne kwa alama 5 nyuma ya Ivory Coast,Gabon na Burundi.
Mchuano huo utarushwa mubashara kupitia runinga ya taifa KBC channel 1.