Timu ya Kenya kwa wanariadha chipukizi yapokea sare

Dismas Otuke
1 Min Read

ITimu ya Kenya kwa wanariadha wasiozidi umri wa miaka 20 imepokea sare kabla ya kuondoka nchini kuelekea Peru kushiriki mashindano ya Dunia wiki ijayo.

Kikosi hicho ambacho kimekuwa kambini katika uwanja wa Kasarani  kwa zaidi ya majuma mawili,  kinawajumuisha wasicha 8 na wavulana 11 na kitaondoka nchini Jumamosi hii kuelekea mjini Lima Peru.

Baadhi ya wanariadha kikosini ni bingwa wa Afrika atika mbio za mita 800 Sarah Moraa, na mshindi wa nishani ya fedha ya Afrika katika mita  3,000 kuruka viunzi na maji Edmund Serem.

Kenya italenga kuboresha matokeo ya mwaka 2022 mjini Cali,Colombia ilikozoa dhahabu 3 fedha 3 na shaba 4.

Mkurugenzi wa Riadha ya Chipukizi  Barnaba Korir alikabidhi sare na viatu kwa timu hiyo siku ya Alhamisi.

 

Share This Article