Kikosi cha Kenya kwa mbio za dunia za kupokezana kijiti kitabainika Jumamosi wakati wa majaribio ya kitaifa katika uwanja wa taifa wa Nyayo.
Mbio za dunia za kupokezana kijiti zitaandaliwa mjini Nassau,Bahamas tarehe 4 na 5 mwezi ujao.
Majaribio hayo yatashirikisha mbio za mita 400,200 na 100 na kisha baadaye majaribio ya mita 400 kwa wanariadha wanne wanaume na pia wanawake,mita 400 kupokezana kijiti mseto na mita 100 kwa wanariadha wanne kupokezana wanaume na pia wanawake.
Kenya kwasasa ji ya 15 katika.mbio za mita 400 kwa wanariadha wanne,ya 20 katika mbio za mita 400 mseto huku timu ya wanaume ya mita 100 kwa wanariadha wanne ikishikilia nafasi ya 27 na ya mita 400 wanawake ni ya 25.
Hata hivyo ni timu 14 pekee katika msimamo wa dunia zitakazofuzu kwa Olimpiki.
Jumla ya wanariadha 83 wamealikwa kushiriki majaribio hayo ya siku moja akiwemo bingwa wa Jumuiya ya madola Ferdinand Omanyala.
Wanariadha watakaojumuishwa kikosini watapata fursa ya kutafuta muda wa kufuzu kwa michezo ya Olimpiki ya jijini Paris Ufaransa.