Timu 70 zafuzu kwa michezo ya Olimpiki kupokezana kijiti huku Kenya ikiambulia pakavu

Dismas Otuke
1 Min Read

Jumla ya timu 70 zilijikatia tiketi kwa michezo ya Olimpiki katika mbio za kupokezana kijiti wakati wa makala ya sita, ya mbio za kupokezana vijiti duniani yaliyoandaliwa baina ya Mei 5 na 6 mjini Nassau,Bahamas.

Timu 40 zilifuzu siku ya Jumamosi huku 30 zikifuzu Jumapili katika suku ya mwisho ya mashindano hayo.

 

Marekani ilinyakua dhahabu nne katika mashindani hayo huku timu ya mita 100 kwa wanariadha wanne na ile ya mita 400 kwa wanariadha wanne, kupokezana kijiti zikivunja rekodi ya mashindano.

Uingereza na Marekani zilishinda dhahabu katika fainali zote za mashindano hayo huku Ufaransa ,Ujerumani ,Italia, Jamaica, Nigeria na Poland zikishinda dhahabu nne.

Kenya ilishiriki katika mbio za mita 400 kwa wanariadha wanne kupokezana kijiti kwa wanaume na wanawake,mita 400 msero na mita 100 kwa wanariadha wanne kupokezana kijiti kwa wanaume.

Share This Article