Tiketi za mchuano wa ufunguzi wa kundi A kuwania kombe la CHAN kati ya Kenya na Jamhuri ya Demokrasia ya Congo, Jumapili hii katika uwanja wa Kasarani zimemalizika kuuzwa.
Tiketi hizo za maeneo ya kawaida zilizokuwa zikiuzwa kwa ada ya shilingi 200 na zile za jukwaa za shilingi 500 zimemalizika kuuzwa mapema Jumatatu.
Waandalizi wa michuano ya CHAN ambayo inafanyika nchini Kenya kwa mara ya kwanza walitangaza kuwa tiketi hizo zitauzwa kupitia mtandaoni pekee.
Kenya itamenyana na DRC Jumapili Agosti 3 kaunzia saa tisa alasiri.