Tiger Traffic ndio mabingwa wa kombe la Ismael Kaunti ya Mandera

Tom Mathinji
1 Min Read

Timu ya Tiger Traffic ndio mabingwa wa awamu ya kwanza,  kombe la Ismail, baada ya kuilaza White city mabao 3-1 Kupitia mikwaju ya penalti.

Kufuatia ushindi huo, Tiger Traffic ilizawadiwa shilingi 200,000, katika shindalo hilo linalolenga kuwawezesha vijana wa kaunti hiyo.

White City walioibuka wapili, walituzwa shilingi  100,000, huku Bula Dana waliokuwa wa tatu wakipokea shilingi 50,000.

Katika mashindano hayo Abdiaahid Karo ambaye aliibuka mfungaji bora wa mabao, alizawadiwa shilingi  10,000, huku Abdihamid Carloz akipokea shilingi 10,000 kwa kuwa mchezaji bora naye Lewi wa White City FC alizawadiwa  shilingi 5,000 kwa kuwa mlinda lango bora.

Shindalo hilo linalolenga kuwahusisha vijana wakati wa likizo za shule utaendelea wikendi ijauo katika kaunti mbili ndogo za Mandera Magharibi na Banisa.

Akizungumza wakati wa fainali hizo Katibu Ismail Maalim, alidokeza kuwa mashindano hayo yanalenga kuwaepusha vijana dhidi ya matumizi ya mihadarati.

“Mashindano haya sio tu kuhusu soka, lakini kuwapa vijana fursa ya kujiimarisha maishani,” alisema Ismail.

Jumla ya timu 66 kutoka kaunti ndogo tatu zinashiriki katika awamu hiyo ya kwanza ya mashindano hayo.

Awamu ya pili itaandaliwa wakati wa likizo wa mwezi Disemba huku kaunti ndogo za Mandera Mashariki , Mandera Kaskazini, na Lafey.

 

 

 

 

 

 

TAGGED:
Share This Article